Kwa zaidi ya miaka 50 wanaharakati wa haki za wanyama wamekuwa wakipambana kuinusuru Serengeti. Lakini mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa idadi ya watu na ujangili vimeiaathiri pakubwa mbuga hii ambayo ni mkusanyiko wa spishi mbalimbali za wanyamapori barani Afrika.
Njoo ujiunge nasi katika safari ndani ya pepo hii ya wanyama ya Tanzania yenye kuvutia lakini inayokabiliwa na kitisho. Tunakupeleka pamoja nasi katika ulimwengu wa kuvutia: Jionee simba wanaounguruma, pundamilia wanaobweka na maelfu ya nyumbu - katika safari yetu ndani ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment