Sunday, 19 June 2016

KOCHA MKUU WA YANGA ASEMA ANAIMANI NA KIKOSI CHAKE CHA LEO DHIDI YA MO BEJAIA


KOCHA mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm amesema kuwa ana imani na kikosi chake kuwa kitacheza vizuri kwani ameweza kukaa nao kwa siku kadhaa na amewapa mbinu mbalimbali hasa wanapokuwa wapo ugenini na zaidi amewataka kutokufuata mchezo wa wapinzani wao.
Pluijm amesema hayo kupitia kwenye mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na kusema wameenda nchini Algeria kwa ushindi ila hawatataka kupoteza mchezo huo zaidi ushindi ndio wanachokitaka au kupata sare ambayo itakuwa na manufaa kuliko kupoteza kabisa.
"Siku chache nilizokaa na wachezaji na wakafanya mazoezi ya pamoja yanatosha kabisa kuweza kuondoka na ushindi kwani Nimewaambia wacheze mchezo wetu na zaidi wasiwafuate mchezo wao,"amesema Pluijm. Ninachoamini kuwa wachezaji wangu watafuata kile nachowaambia na zaidi wapinzani wangu watatumia uwanja wao wa nyumbani kucheza kwa kujiamini na sisi tutacheza kwa tahadhari kubwa sana.
Yanga wanacheza leo na Mo Bejaia ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa kundi A ambao utapigwa nchini Algeria saa sita na robo usiku wa saa za Afrika Mashariki. Katika mchezo huo watakosa huduma ya Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro' anayetumikia kadi nyekundu na Juma Abdul ambaye ni majeruhi.

No comments:

Post a Comment